Friday, March 27, 2009

lukwangule entertainment: Kova azungumzia ajali ya mheshimiwa Chenge

lukwangule entertainme

Kamanda wa Polisi wa kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam Suleiman Kova (pichani) mchana huu aliunguruma Central polisi kuhusiana na suala la mheshimiwa Andrew Chenge kugonga na kuua watu wawili alfajiri leo.
Kamanda Kova alisema kwamba mheshimiwa mbunge huyo alipata ajali hiyo majira ya saa kumi alfajiri akiwa anaendesha pick up Hilux namba T 512 ACE.
Amesema akitokea njia panda inayoingilia St peters kuelekea Morogoro Store, mheshimiwa Chenge akiwa shule ya Msingi ya osyterbay barabara ya Karume na Haile Sellasie gari yake iligongana na Bajaj no T 736 AXE iliyokuwa inatokea Morogoro store.
Kova alisema bajaj hiyo ilikuwa na watu watatu dereva mmoja na wanawake wawili ambao walikufa palepale na dereva hajulikani alipo.
Amesema kwamba wanawake hao wawili wanaumri kati ya miaka 20 na 28 na majina yao bado kufahamika. maiti za wasichana hao zimehifadhiwa hospitali ya mwananyamala.
Imeelezwa kuwa mheshimiwa chenge anaendelea kuisaidia Polisi.
polisi imesema kwamba baja hiyo ni mali ya Zuwena Feith Nassoro wa SLP 2595 Dar es salaam.nt: Kova azungumzia ajali ya mheshimiwa Chenge

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.comme google-site-verification=Qm-XNfnL5kai8WV2inT1RRX2WIPaBTG_WPq3kYSBwbgKennedy Kimaro 2008 NYUMBANI NI NYUMBANI TU KUMBUKA KUWEKEZA NYUMBANI LEO

Rudi TOP-Juu